Sheria ilimbana mgombea ubunge wa Afrika Mashariki Rose Daudi Mwalusamba ambae alitangaza uamuzi wa kujitoa kugombea nafasi hiyo baada ya kushindwa kujieleza vizuri mbele ya Wabunge.
Hilo limetangazwa wakati wa mchakato wa kuwatafuta wabunge wa Afrika Mashariki ambapo wagombea mbalimbali walizitoa sera zao kwa lugha ya kiingereza kwenye bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania April 17 2012.
Kauli aliyoitoa kwa kiingereza mbunge Rose Mwalusamba kuhusu kujiondoa, sauti yake iko hapo chini unaweza kuisikiliza.
Hata hivyo washindi wa Ubunge huo ni Shayrose Banji,Anjela Charless Kizigha,Mwinyi Hassan,Taslim Twaha Issa, Kesi Ndelakindo Perepetua, Kimbisa Adam Omary,Murunya Bernad,Makongoro Nyerere na Yahya kwa mujibu wa mrokim.blogspot.com
Kabla ya wabunge hao
kutangazwa, Mbunge wa Kyela Mh Harrison Mwakyembe alisimama na
kuzungumza bungeni kwa kutoa kauli ifuatayo “Muheshimiwa spika lazima
niseme ukweli kwamba heshima yetu ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki
kwa kiasi, imemomonyoka sana kutokana na baadhi ya wawakilishi
tunaowachagua hapa kuwa chini ya kiwango, hawana uwezo, kwa hiyo wanakua
mabubu katika kipindi chote cha uwakilishi wao, watu wanajua tu kuomba
kura na kupiga magoti, wakifika kule voice of Kenya kuna interview
wamejificha chini ya meza wanabakia watu watatu tu kuongea, waheshimiwa
wabunge nawaomba tuchague watu wenye uwezo”
No comments:
Post a Comment