Thursday, March 22, 2012

Mlima Kilimanjaro


 Mlima huu ni mojawapo ya vitambulisho muhimu sana vya nchi yetu. Ukisikia The Land of Kilimanjaro unajua nini kinaongelewa. Matangazo ya televisheni ambayo yamekuwa yakionekana hivi karibuni katika vituo mbalimbali vya televisheni Ulaya na Marekani ya Kaskazini hususani CNN,huenda yakasaidia kuukumbusha ulimwengu na pia jirani zetu kwamba Mlima Kilimanjaro upo kaskazini mwa Tanzania na si vinginevyo. Mtu ambaye anapewa heshima ya kuwa mtu wa kwanza aliitwa Yohani Kinyala Lauwo (baadaye alijulikana zaidi kama Mzee Lauwo). Cha ajabu alipomsindikiza mzungu wa kwanza kuupanda Mlima mjerumani aliyeitwa Hans Meyer, vitabu vya historia (potofu) vikampa sifa zote Hans Meyer. Mzee Lauwo alizaliwa mwaka 1872 na akafariki mwaka 1996. Unaweza kusoma kuhusu historia hii zaidi kwa kubonyeza hapa.

No comments: